TEKNOLOJIA YA NDEGE ZISIZO NA RUBANI: UTENGENEZAJI NA UTUMIAJI WAKE KATIKA UCHORAJI WA RAMANI ZITUMIKAZO KATIKA UTOAJI WA MISAADA YA KIBINADAMU NA MAENDELEO YA JAMII YA KITANZANIA

Matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yamekuwa muhimu sana kwa utoaji wa misaada ya kibinadamu haswa katika utoaji wa huduma za kiafya haswa katika usambazaji wa madawa muhimu kwa uharaka mahali pasipofikika kwa urahisi. Kutokana na umuhimu huo sisi “HOT TANZANIA” tumeona muhimu kwa upande mwingine wa kutengeneza ndege hizo nchini Tanzania na kuzitumia kwa upigaji picha zitakazotumika katika uchoraji wa ramani ili kupata ramani za kisasa ambazo zitaweza kusaidia katika utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na kukuza maendeleo kwa njia ya data zitokanazo kwa uchambuzi wa Ramani.

Ingawa kuna picha za satelaiti ambazo hupatikana bila gharama lakini unakuta zimepigwa kwa muda mrefu ama zinakuwa na mawingu yanayokuwa yamefunika uso wa dunia kutokana na satelaiti kuwa nje ya dunia juu ya mawingu hivyo unakuta hazifai kwa ramani za wakati huu, hivyo ikiwa unatumia picha ya satellite katika uandaaji wa ramani itakulpatia ramani ya wakati huo wakati picha imechukuliwa. Kwa hivyo ili kuwa na ramani ya uso wa dunia wa kipindi cha hivi karibuni ni vyema ikapatikana picha ya hivi karibuni ili kuwezesha kuongeza taarifa zilizoongezeka katika uso wa dunia zitokanazo na mabadiliko yanayosababishwa na shughuli za kibinaadamu kwa kutumia vyombo virukavyo chini ya mawingu vya gharama nafuu zijulikanazo kama Ndege zisizo na rubani (Drones) ili kupata picha yenye muonekano mzuri zitakazokuwa na msaada wa upatikanaji wa ramani zenye taarifa za wakati huu zitakazokuwa na misaada mbalimbali kwa jamii ya Kitanzania na mahali pengine kama teknolojia hii ukitumiwa.

Kulingana na lengo la shirika hili lihusikalo na uchoraji wa ramani huru zitakazosaidia kwa shughuli za misaada ya kibinadamu na udhibiti wa maafa “HOT”, changamoto tunayokabiliana kwa sasa katika upatikanaji picha ya wakati huu itakayosaidia katika uchoraji wa ramani yenye taarifa za wakati huu, Hivyo tumeona ni vyema kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani (Drones) ambayo tutakuwa tunazitengeneza hapa hapa nchini na kuzitumia katika upigaji picha (kama lengo la msingi) zenye kumbukumbu za kijiografia zitakazosaidia kupatikana kwa ramani ya kisasa zaidi.

Zaidi ya hayo, kutokana na uhafifu wa upatikanaji wa rasilimali za kuunga mkono teknolojia ya ndege zisizo na rubani, tunapenda kuwakaribisha sana Wadau mbalimbali wa kimaendeleo katika kusaidia juhudi zetu kuendelea mbele kwa maendeleo ya jamii ya kiTanzania kupitia teknolojia hii.

Kwa maelezo ya picha/video kuhusu utengenezaji wa ndege hizi na majaribuo yake tafadhali bonyeza hapa chini

Majaribio ya nje (video)

Majaribio ya ndani (video)

Maandalizi kwa majaribio ya asubuhi (Picha)

 

Advertisements

Author: bornlove

Open Knowledge enthusiast

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s